16 wa Ido, Zekaria; wa Ginethoni, Meshulamu;
17 wa Abiya, Zikri; ukoo wa Miniamini; wa Moadia, Piltai;
18 wa Bilga, Shamua; wa Shemaya, Yehonathani;
19 wa Yoaribu, Matenai; wa Yedaya, Uzi;
20 wa Salai, Kalai; wa Amoki, Eberi;
21 wa Hilkia, Heshabia; na wa ukoo wa Yedaya, Nethaneli.
22 Wakati wa Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua wakuu wa jamaa za Walawi, waliorodheshwa; vilevile wakati wa utawala wa mfalme Dario wakuu wa jamaa za makuhani waliorodheshwa.