5 Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu ili kujua koo zao. Nikapata kitabu cha koo za watu waliorudi toka uhamishoni mara ya kwanza, na hawa wafuatao ndio waliokuwa wameorodheshwa ndani yake.
6 Wale waliokuwa uhamishoni kule Babuloni, walirudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda, kila mmoja akarudi mjini kwake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babuloni tangu mfalme Nebukadneza alipowahamishia huko wakiwa mateka.
7 Waliporudi waliongozwa na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Misperethi, Bigwai, Nehumu na Baana. Ifuatayo ni idadi ya watu wa koo za Israeli waliorudi toka uhamishoni:
8 Watu wa ukoo wa Paroshi: 2,172;
9 wa ukoo wa Shefatia: 372;
10 wa ukoo wa Ara: 652;
11 wa ukoo wa Pahath-moabu, yaani wazawa wa Yeshua na Yoabu: 2,818;