15 Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu,ni siku ya dhiki na uchungu,siku ya giza na huzuni;siku ya uharibifu na maangamizi,siku ya mawingu na giza nene.
16 Siku hiyo ni ya mlio wa tarumbeta ya vita,dhidi ya miji yenye ngome na kuta ndefu.
17 Kwa kuwa watu wamemkosea Mwenyezi-Mungu,yeye atawaletea dhiki kubwa,hivyo kwamba watatembea kama vipofu.Damu yao itamwagwa kama vumbi,na miili yao kama mavi.
18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoakatika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.Kwa moto wa wivu wakedunia yote itateketezwa.Kwa ukamilifu na kwa namna ya kutishaatawafanya wakazi wote duniani watoweke.