11 Baada ya Ibzani, Eloni wa kabila la Zebuluni, akawa mwamuzi wa Israeli kwa miaka kumi.
12 Naye akafariki, akazikwa mjini Aiyaloni katika nchi ya kabila la Zebuluni.
13 Baada ya Eloni, Abdoni mwana wa Hileli kutoka Pirathoni akawa mwamuzi wa Israeli.
14 Yeye alikuwa na watoto wa kiume arubaini na wajukuu thelathini ambao walipanda punda sabini. Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka minane.
15 Kisha Abdoni akafariki, akazikwa mjini Pirathoni katika nchi ya kabila la Efraimu kwenye eneo la milima ya Waamaleki.