1 Naingia bustanini mwangu,dada yangu, bi arusi.Nakusanya manemane na viungo,nala sega langu la asali,nanywa divai yangu na maziwa yangu.Kuleni enyi marafiki, kunyweni;kunyweni sana wapendwa wangu.
2 Nililala, lakini moyo wangu haukulala.Sauti ya mpenzi wangu anabisha hodi.“Nifungulie, dada yangu mpenzi wangu, bibiarusi wangu,hua wangu, usiye na kasoro.Kichwa changu kimelowa umandena nywele zangu manyunyu ya usiku.”
3 Nimekwisha yavua mavazi yangu,nitayavaaje tena?Nimekwisha nawa miguu yangu,niichafueje tena?
4 Hapo mpenzi wangu akaugusa mlango,moyo wangu ukajaa furaha.
5 Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu.Mikono yangu imejaa manemane,na vidole vyangu vyadondosha manemane,nilipolishika komeo kufungua mlango.
6 Nilimfungulia mlango mpenzi wangu,lakini kumbe, alikuwa amekwisha toweka.Moyo wangu ulifurahi alipokuwa akizungumza!Nilimtafuta, lakini sikumpata;nilimwita, lakini hakuniitikia.