1 “Wakati huo na siku hizonitakapoirekebisha hali ya Yuda na Yerusalemu,
2 nitayakusanya mataifa yote,niyapeleke katika bonde liitwalo,‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu.Huko nitayahukumu mataifa hayo,kwa mambo yaliyowatendea watu wangu Israeli,hao walio mali yangu mimi mwenyewe.Maana waliwatawanya miongoni mwa mataifa,waligawa nchi yangu
3 na kugawana watu wangu kwa kura.Waliwauza wavulana ili kulipia malaya,na wasichana ili kulipia divai.
4 “Mnataka kunifanya nini enyi Tiro na Sidoni na maeneo yote ya Filistia? Je, mna kisasi nami mnachotaka kulipiza? Kama mnalipiza kisasi, mimi nitawalipizeni mara moja!