18 “Wakati huo, milima itatiririka divai mpya,na vilima vitatiririka maziwa.Vijito vyote vya Yuda vitajaa maji;chemchemi itatokea nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu,na kulinywesha bonde la Shitimu.
19 “Misri itakuwa mahame,Edomu itakuwa jangwa tupu,kwa sababu waliwashambulia watu wa Yudawakawaua watu wasio na hatia.
20 Bali Yuda itakaliwa milele,na Yerusalemu kizazi hata kizazi.
21 Nitawaadhibu waliomwaga damu ya watu wa Yudawala sitawaachia wenye hatia.Mimi, Mwenyezi-Mungu nakaa Siyoni.”