1 Sehemu waliyogawiwa wazawa wa Yosefu kwa kura ilianzia karibu na mto Yordani, mashariki ya chemchemi ya Yeriko, na kupitia jangwani, hadi kwenye sehemu za milima mpaka Betheli.
2 Kutoka Betheli mpaka ulielekea Luzu ukapita Atarothi ambako waliishi Waarki.
3 Kisha ukashuka magharibi katika nchi ya Wayafleti hadi Beth-horoni ya Chini na Gezeri na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea.
4 Wazawa wa Yosefu, yaani kabila la Manase na kabila la Efraimu, walipewa nchi hiyo kuwa milki yao.