1 Fungua milango yako, ewe Lebanoniili moto uiteketeze mierezi yako!
2 Ombolezeni, enyi misunobari,kwa kuwa mierezi imeteketea.Miti hiyo mitukufu imeharibiwa!Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni,kwa kuwa msitu mnene umekatwa!
3 Sikia maombolezo ya watawala!Fahari yao imeharibiwa!Sikia ngurumo za simba!Pori la mto Yordani limeharibiwa!
4 Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, alisema hivi: “Jifanye mchungaji wa kondoo waendao kuchinjwa.