1 Yule malaika aliyeongea nami, akanijia tena, akaniamsha kama kumwamsha mtu usingizini.
2 Akaniuliza, “Unaona nini?” Nami nikamjibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu. Juu yake kuna bakuli la mafuta na taa saba, na kila moja ina mahali pa kutilia tambi saba.
3 Karibu na kinara hicho kuna miti miwili ya mzeituni; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.”
4 Basi, nikamwuliza huyo malaika, “Bwana, vitu hivi vinamaanisha nini?”
5 Naye akanijibu, “Hujui vitu hivi vinamaanisha nini?” Nikamjibu, “Sijui bwana.”