1 Niliona maono mengine tena. Safari hii, niliona magari manne ya farasi yakitoka katikati ya milima miwili ya shaba nyeusi.
2 Gari la kwanza lilikokotwa na farasi wekundu, la pili lilikokotwa na farasi weusi,
3 la tatu lilikokotwa na farasi weupe, na la nne lilikokotwa na farasi wa kijivujivu.
4 Basi, nikamwuliza yule malaika aliyeongea nami, “Bwana, magari haya ya farasi yanamaanisha nini?”