4 Basi, nikamwuliza yule malaika aliyeongea nami, “Bwana, magari haya ya farasi yanamaanisha nini?”
5 Malaika akanijibu, “Magari haya ni pepo kutoka pande nne za mbingu. Yalikuwa mbele ya Mwenyezi-Mungu wa dunia nzima, na sasa yanaondoka.
6 Lile gari linalokokotwa na farasi weusi linakwenda kaskazini, lile linalokokotwa na farasi weupe linakwenda magharibi, na lile linalokokotwa na farasi wa kijivujivu linakwenda kusini.”
7 Farasi hao walipotokea walikuwa na hamu sana ya kwenda kuikagua dunia. Naye malaika akawaambia, “Haya! Nendeni mkaikague dunia.” Basi, wakaenda na kuikagua dunia.
8 Kisha yule malaika aliyeongea nami akaniambia kwa sauti, “Tazama! Wale farasi waliokwenda nchi ya kaskazini wameituliza ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.”
9 Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
10 “Pokea zawadi za watu walio uhamishoni zilizoletwa na Heldai, Tobia na Yedaya. Nenda leo hii nyumbani kwa Yosia, mwana wa Sefania ambamo watu hao wamekwenda baada ya kuwasili kutoka Babuloni.