8 Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme.
9 Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii.
10 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,Tazama, mimi namtuma mjumbe wanguMbele ya uso wako,Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.
12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.