1 Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema,Sauti ya mtu aliaye nyikani,Itengenezeni njia ya Bwana,Yanyosheni mapito yake.
4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;