12 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;
13 akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
14 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
15 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani,Galilaya ya mataifa,
16 Watu wale waliokaa katika gizaWameona mwanga mkuu,Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mautiMwanga umewazukia.
17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
18 Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.