1 Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;
2 wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.
3 Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu BWANA.
4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;