2 Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema,
3 Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema,
4 BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya BWANA, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.
5 Naye Rehoboamu akakaa Yerusalemu, akajenga miji yenye ngome katika Yuda.
6 Akajenga na Bethlehemu, na Etamu, na Tekoa,
7 na Bethsuri, na Soko, na Adulamu,
8 na Gathi, na Maresha, na Zifu,