2 Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka binti Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
3 Abiya akapanga vita mwenye jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule mia nne elfu; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake mwenye watu wateule mia nane elfu, waliokuwa waume mashujaa.
4 Basi Abiya akasimama juu ya kilima cha Semaraimu, kilichoko milimani mwa Efraimu, akasema, Nisikieni, enyi Yeroboamu na Israeli wote;
5 je! Haikuwapasa kujua ya kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?
6 Lakini Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumwa wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka, akamfanyia fitina bwana wake.
7 Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia.
8 Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa BWANA mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu.