11 Tena angalieni, Amaria, kuhani mkuu, yu juu yenu kwa maneno yote ya BWANA; naye Zebadia, mwana wa Ishmaeli, jemadari wa nyumba ya Yuda, kwa maneno yote ya mfalme; Walawi nao watakuwa wasimamizi mbele yenu. Jitieni nguvu, mtende, naye BWANA awe pamoja nao walio wema.