1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala miaka arobaini huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote za Yehoyada kuhani.
3 Yehoyada akamwoza wake wawili, naye akazaa wana na binti.
4 Ikawa baada ya haya, Yoashi alikuwa na nia ya kuitengeneza nyumba ya Mungu.