22 Ndipo kwato za farasi zilikanyaga-kanyagaKwa sababu ya kupara-para,Kupara-para kwao wenye nguvu.
23 Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA,Walaanini kwa uchungu wenyeji wake;Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA,Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.
24 Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote;Mkewe Heberi, Mkeni,Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani.
25 Aliomba maji, naye akampa maziwa.Akamletea siagi katika sahani ya heshima.
26 Akanyosha mkono wake akashika kigingi,Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi;Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake.Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake.
27 Miguuni pake aliinama, akaanguka, akalala.Miguuni pake aliinama, akaanguka.Hapo alipoinama, ndipo alipoanguka amekufa.
28 Alichungulia dirishani, akalia,Mama yake Sisera alilia dirishani;Mbona gari lake linakawia kufika?Mbona gurudumu za gari lake zinakawia?