39 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaombolea sana.
40 Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.
41 Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyahalifu maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.
42 Msikwee, kwa kuwa BWANA hamo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu.
43 Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimwandame BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi.
44 Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la agano la BWANA halikutoka humo maragoni, wala Musa hakutoka.
45 Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakatelemka, wakawapiga na kuwaangusha, hata kufikilia Horma.