7 Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania.
8 Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa malozi mabivu.
9 Kisha Musa akazileta nje hizo fimbo zote kutoka hapo mbele za BWANA na kuziweka mbele ya wana wa Israeli wote; nao wakaangalia, na kila mtu akaitwaa fimbo yake.
10 Kisha BWANA akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung’uniko yao waliyoninung’unikia, ili wasife.
11 Basi Musa akafanya vivyo; kama BWANA alivyomwagiza, ndivyo alivyofanya.
12 Kisha wana wa Israeli wakanena na Musa, na kumwambia, Angalia, sisi twafa, twaangamia, sote twaangamia.
13 Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa pia sote?