10 Kisha wana wa Israeli wakasafiri, wakapanga marago Obothi.
11 Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika jangwa iliyoelekea Moabu, upande wa maawio ya jua.
12 Kutoka huko wakasafiri, wakapanga katika bonde la Zeredi.
13 Kutoka huko wakasafiri, wakapanga upande wa pili wa Arnoni, ulio jangwani, utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
14 Kwa hiyo imesemwa katika chuo cha Vita vya BWANA,Wahebu katika Sufa,Na bonde za Arnoni,
15 Na matelemko ya hizo bondeKwenye kutelemkia maskani ya Ari,Na kutegemea mpaka wa Moabu.
16 Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri; ni kisima ambacho BWANA alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.