1 Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani.
2 Balaamu akainua macho yake akawaona Israeli wamekaa kabila kabila; roho ya Mungu ikamjia.
3 Akatunga mithali yake, akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema;
4 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho;
5 Mahema yako ni mazuri namna gani, Ee Yakobo,Maskani zako, Ee Israeli!