3 Akatunga mithali yake, akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema;
4 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho;
5 Mahema yako ni mazuri namna gani, Ee Yakobo,Maskani zako, Ee Israeli!
6 Mfano wa bonde zimetandwa,Mfano wa bustani kando ya mto,Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA,Mfano wa mierezi kando ya maji.
7 Maji yatafurika katika ndoo zake,Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi.Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi,Na ufalme wake utatukuzwa.
8 Mungu amemleta kutoka Misri,Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati;Atawameza mataifa walio adui zake,Ataivunja mifupa yao vipande vipande.Atawachoma kwa mishale yake.
9 Aliinama, akalala mfano wa simba,Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha?Na abarikiwe kila akubarikiye,Na alaaniwe kila akulaaniye.