66 Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, mkuu wa wana wa Dani;
67 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
68 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;
69 na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;
70 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;
71 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.
72 Na siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Asheri;