12 Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo BWANA, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa,
13 Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua;
14 ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii; nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano wa haya yafanyika katikati yako;
15 hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga.
16 Na nyara zake zote uzikusanyie katikati ya njia yake; na mji uuteketeze kwa moto, na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa BWANA, Mungu wako; nao utakuwa magofu milele; usijengwe tena.
17 Kisishikamane na mkono wako kitu cho chote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke BWANA na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako;
18 utakaposikiza sauti ya BWANA, Mungu wako kwa kushika maagizo yake yote nikuagizayo leo, ufanye yaliyoelekea machoni pa BWANA, Mungu wako.