16 na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa;
17 na mwari, na nderi, na mnandi;
18 na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo.
19 Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.
20 Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
21 Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.