6 na wazee wote wa mji ule, ulio karibu sana na yule aliyeuawa, na waoshe mikono yao juu ya huyo mtamba aliyevunjwa shingo yake humo bondeni;
7 na wajibizane kwamba, Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuiona.
8 Ee BWANA, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao.
9 Ndivyo utakavyoondoa damu ya asiye makosa katikati yako, utakapofanya yaliyo sawa machoni pa BWANA.
10 Utakapokwenda vitani kupigana juu ya adui zako, na BWANA, Mungu wako, awatiapo mikononi mwako, nawe uwachukuapo mateka,
11 ukaona kati ya mateka mwanamke mzuri, ukafanya tamaa kwake, ukawaza kumtwaa kuwa mkeo;
12 ndipo umchukue kwenu nyumbani kwako, naye atanyoa kichwa, akate na kucha;