1 Musa akaenda akawaambia Waisraeli maneno haya yote.
2 Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia na ishirini; siwezi tena kutoka na kuingia, na BWANA ameniambia, Hutavuka mto huu Yordani.
3 BWANA Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama BWANA alivyonena.
4 Na BWANA atawatenda hao kama vile alivyowatenda Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, na nchi yao, ambao aliwaharibu.