24 Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto,Na uharibifu mkali;Nitawapelekea meno ya wanyama wakali,Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.
25 Nje upanga utawafifilizaNa ndani ya vyumba, utisho;Utaangamiza mvulana na msichana,Anyonyaye pamoja na mwenye mvi,
26 Nalisema, Ningewatawanyia mbali,Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;
27 Isipokuwa naliogopa makamio ya adui,Adui zao wasije wakafikiri uongo,Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka,Wala BWANA hakuyafanya haya yote.
28 Maana hawa ni taifa wasio shauri,Wala fahamu hamna ndani yao.
29 Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya,Ili watafakari mwisho wao.
30 Mmoja angefukuzaje watu elfu,Wawili wangekimbizaje elfu kumi,Kama Mwamba wao asingaliwauza,Kama BWANA asingaliwatoa?