35 Kisasi ni changu mimi, na kulipa,Wakati itakapoteleza miguu yao;Maana siku ya msiba wao imekaribia,Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.
36 Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,Atawahurumia watumwa wake,Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka,Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,
37 Naye atasema, Iko wapi miungu yao,Mwamba ule walioutumaini;
38 Uliokula shahamu za sadaka zao,Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji?Na waondoke na kuwasaidia ninyi;Na wawe hao himaya yenu.
39 Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye,Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi;Naua Mimi, nahuisha Mimi,Nimejeruhi, tena naponya;Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,
40 Maana, nainua mkono wangu mbinguni,Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,
41 Nikiunoa upanga wangu wa umeme,Mkono wangu ukishika hukumu,Nitawatoza kisasi adui zangu,Nitawalipa wanaonichukia.