4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu;Maana, njia zake zote ni haki.Mungu wa uaminifu, asiye na uovu,Yeye ndiye mwenye haki na adili.
5 Wametenda mambo ya uharibifu,Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao;Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.
6 Je! Mnamlipa BWANA hivi,Enyi watu wapumbavu na ujinga?Je! Yeye siye baba yako aliyekununua?Amekufanya, na kukuweka imara.
7 Kumbuka siku za kale,Tafakari miaka ya vizazi vingi;Mwulize baba yako, naye atakuonyesha;Wazee wako, nao watakuambia.
8 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao,Alipowabagua wanadamu,Aliweka mipaka ya watuKwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
9 Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake,Yakobo ni kura ya urithi wake.
10 Alimkuta katika nchi ya ukame,Na katika jangwa tupu litishalo;Alimzunguka, akamtunza;Akamhifadhi kama mboni ya jicho;