1 Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda.
2 BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu.
3 BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai.
4 BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto;
5 (nami wakati ule nalisimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonyesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema,
6 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.