13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa,Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.
14 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka,Wakaao Ufilisti utungu umewashika.
15 Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa,Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata,Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.
16 Hofu na woga umewaangukia;Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe;Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA,Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.
17 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako,Mahali pale ulipojifanyia, Ee BWANA, ili upakae,Pale patakatifu ulipopaweka imara, BWANA, kwa mikono yako.
18 BWANA atatawala milele na milele.
19 Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.