8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
9 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara,Nafsi yangu itashibishwa na wao;Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
11 Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe?Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu,Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
12 Ulinyosha mkono wako wa kuume,Nchi ikawameza.
13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa,Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.
14 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka,Wakaao Ufilisti utungu umewashika.