1 Tupa chakula chako usoni pa maji;Maana utakiona baada ya siku nyingi.
2 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane;Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.
3 Mawingu yakiwa yamejaa mvua,Yataimimina juu ya nchi;Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini,Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.
4 Mwenye kuuangalia upepo hatapanda;Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
5 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
6 Asubuhi panda mbegu zako,Wala jioni usiuzuie mkono wako.Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
7 Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua.