10 Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe;Katika Beth-le-Afra ugae-gae mavumbini.
11 Piteni; uende ukaaye Shafiri, hali ya uchi na aibu;Hivyo akaaye Saanani hajatokea nje;Maombolezo ya Beth-eseli yatawaondolea tegemeo lake;
12 Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema;Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa BWANA,Umefika mpaka lango la Yerusalemu.
13 Mfungie gari la vita farasiAliye mwepesi, ukaaye Lakishi;Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni;Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.
14 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia;Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.
15 Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki;Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu.
16 Jifanyie upaa, jikate nywele zako,Kwa ajili ya watoto waliokufurahisha;Panua upaa wako kama tai;Kwa maana wamekwenda mbali nawe utumwani.