3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4 Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
5 Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
7 Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
8 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.