1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi