3 na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi.
4 Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli.
5 Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani.
6 Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng’ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.
7 Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.
8 Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.
9 Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri.