6 BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
10 Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi.
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.
12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.