5 Na baada yao wakafanyiza Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao.
6 Na lango la kale wakalifanyiza Yoyada, mwana wa Pasea, na Meshulamu, mwana wa Besodeya; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.
7 Na baada yao wakafanyiza Melatia, Mgibeoni, na Yadoni, Mmeronothi, watu wa Gibeoni, na wa Mispa, raia wa kiti cha enzi cha liwali wa ng’ambo ya Mto.
8 Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.
9 Na baada yao akafanyiza Refaya, mwana wa Huri, akida wa nusu ya Yerusalemu.
10 Na baada yao akafanyiza Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akafanyiza Hatushi, mwana wa Hashabneya.
11 Malkiya, mwana wa Harimu, na Hashubu, mwana wa Pahath-moabu, wakafanyiza sehemu nyingine, na mnara wa tanuu.