2 Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa;Umedharauliwa sana.
3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,Wewe ukaaye katika pango za majabali,Mwenye makao yako juu sana;Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
4 Ujapopanda juu kama tai,Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota,Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
5 Kama wevi wangekujilia, kama wanyang’anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe?
6 Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa!
7 Watu wote wa mapatano yakoWamekufukuza, hata mipakani;Wale waliofanya amani naweWamekudanganya, na kukushinda;Walao mkate wako wameweka mtego chini yako;Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
8 Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.