13 Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu,Nao umeishinda;Ametandika wavu aninase miguu,Amenirudisha nyuma;Amenifanya kuwa mtu wa pekee,Na mgonjwa mchana kutwa.
14 Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake;Hayo yameshikamana;Yamepanda juu shingoni mwangu;Amezikomesha nguvu zangu;
15 Bwana amenitia mikononi mwao,Ambao siwezi kupingamana nao.Bwana amewafanya mashujaa wangu woteKuwa si kitu kati yangu;Ameita mkutano mkuu kinyume changuIli kuwaponda vijana wangu;Bwana amemkanyaga kama shinikizoniHuyo bikira binti Yuda.
16 Mimi ninayalilia mambo hayo;Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji;Kwa kuwa mfariji yu mbali nami,Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi;Watoto wangu wameachwa peke yao,Kwa sababu huyo adui ameshinda.
17 Sayuni huinyosha mikono yake;Hakuna hata mmoja wa kumfariji;BWANA ametoa amri juu ya Yakobo,Kwamba wamzungukao wawe watesi wake;Yerusalemu amekuwa kati yaoKama kitu kichafu.
18 BWANA ndiye mwenye haki;Maana nimeiasi amri yake;Sikieni, nawasihi, enyi watu wote,Mkayatazame majonzi yangu;Wasichana wangu na wavulana wanguWamechukuliwa mateka.
19 Naliwaita hao walionipendaLakini walinidanganya;Makuhani wangu na wazee wanguWalifariki mjini;Hapo walipokuwa wakitafuta chakulaili kuzihuisha nafsi zao.