19 Waliotufuatia ni wepesiKuliko tai za mbinguni;Hao walitufuatia milimani,Nao walituotea jangwani.
20 Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA,Alikamatwa katika marima yao;Ambaye kwa habari zake tulisema,Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.
21 Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu,Ukaaye katika nchi ya Usi;Hata kwako kikombe kitapita,Utalewa, na kujifanya uchi.
22 Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni;Hatakuhamisha tena;Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu;Atazivumbua dhambi zako.