1 Wimbo ulio bora, wa Sulemani.
2 Kubusu na anibusu kwa kinywa chake.Maana pambaja zako zapita divai;
3 Manukato yako yanukia vizuri;Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa;Kwa hiyo wanawali hukupenda.
4 Nivute nyuma yako, na tukimbie;Mfalme ameniingiza vyumbani mwake.Tutafurahi na kukushangilia;Tutazinena pambaja zako kuliko divai;Ndiyo, ina haki wakupende.
5 Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri,Enyi binti za Yerusalemu,Mfano wa hema za Kedari,Kama mapazia yake Sulemani.
6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi,Kwa sababu jua limeniunguza.Wana wa mamangu walinikasirikia,Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu;Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.