3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu,Na kinywa chako ni kizuri;Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,Uliojengwa pa kuwekea silaha;Ngao elfu zimetungikwa juu yake,Zote ni ngao za mashujaa.
5 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,Nyuma ya barakoa yako.Ambao ni mapacha ya paa;Wakilisha penye nyinyoro.
6 Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie,Nitakwenda kwenye mlima wa manemane,Na kwenye kilima cha ubani.
7 Mpenzi wangu, u mzuri pia pia,Wala ndani yako hamna ila.
8 Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni,Pamoja nami toka Lebanoni.Shuka kutoka kilele cha Amana,Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni;Kutoka mapangoni mwa simba,Kutoka milimani mwa chui.
9 Umenishangaza moyo, umbu langu,Bibi arusi, umenishangaza moyo,Kwa mtupo mmoja wa macho yako,Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.