12 Ameiumba dunia kwa uweza wake,Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake,Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
13 Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni,Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi;Huifanyia mvua umeme,Huutoa upepo katika hazina zake.
14 Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa;Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga;Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo,Wala hamna pumzi ndani yake.
15 Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu;Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.
16 Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;Na Israeli ni kabila ya urithi wake;BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
17 Haya! Kusanya bidhaa yako katika nchi, wewe ukaaye katika mazingiwa.
18 Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.